Monday, June 02, 2008

Sammy Kipterer Korir

"Snitcher" wa polisi

wa wageni Norway



Swali: je, ni wangapi wanalipwa na

polisi kuchunguza Waafrika wenzao?



Sammy Korir. Picha na Dagbaldet.


Gazeti la kila siku la Dagbladet (Norway) limeandika leo maofisa wakuu wawili waandamizi wa polisi kitengo cha wageni wanachunguzwa kwa kumwajiri Sammy Korir bila ya mkuu wa kitengo kuwa na habari zake.

Sammy Korir amekuwa akilipwa kama kachero wa kitengo cha polisi Norway kinachoshughulikia wageni "Politietsutlendingsenhet - PU (kwa Kinorweji)" , licha ya kuwa si polisi na wala si kachero. Korir amekuwa akilipwa kwa kuwafichua wageni wanaoingia Norway kinyemela na kuomba vibali vya kuishi kama wakimbizi au wageni wa kawaida. Korir amedai aliajiriwa toka Februari 2007 hadi Aprili 2008 alipowaandikia PU kuwa anaacha ukachero.

Polisi wa Norway wamekuwa wakipata shida ya kugundua watu waliojilipua kama wakimbizi na baadaya kupotea mitaani. Sammy Korir amewafichua watu 32 walioingia kinyemela na kuomba hifadhi ya kikimbizi. Watu 19 kati ya hao 32, tayari wamesharudishwa makwao. Chanzo chetu kinasema kuwa Korir amekuwa akihoji watu wanaojilipua na kuwatishia wasiposema ukweli atasema wanatoka nchi ambazo hawatoki wakakione. Baadhi ya watu walirudishwa kwenye ambazo hawatoki, na nchi hizo zilikataa kuwapokea watu hao, ikabidi warudishwe Norway.

Sammy Korir amekuwa akilipwa na polisi kuchunguza na kufuatilia nyendo za watu wanaolijipua. Vyanzo vya habari zetu vya kuaminika vinasema kuwa Korir amekuwa akilipwa na polisi kwa muda mrefu sana ili kufuatilia nyendo za Waafrika nchini Norway.

Mkuu wa kitengo hicho, Bi. Ingrid Wirum, anasema kuwa Korir amelipwa 170000,- (laki moja na sabini elfu). Sammy Korir anadai anaidai polisi kroner 200000,- (laki mbili) na kuwa kama hawatamlipa, ataifungulia polisi mashtaka.

Sammy Korir anajulikana hapa Norway kwa utapeli na uongo. Mwaka 1992 Korir alihukumiwa kwa utapeli.

Mwaka 1996 alianzisha Rainbow Foundation. Alipoanzisha, akaandikisha vyama vingi vya Waafrika viko chini ya Rainbow Foundation (Chama Cha Watanzania Oslo kikiwa kimojawapo), bila ya idhini ya hivyo vyama. Korir akaomba pesa za kuendesha chama na vitengo vinavyohusika akapewa. Pesa hazijulikani zilivyotumika. Lengo lingine la Rainbow Foundation lilikuwa kueneza habari juu ya athari za VVU (Virusi Vya Ukimwi) na UKIMWI miongoni mwa vijana wa Kiafrika waishio Stavanger, Bergen, Trondheim na Tromsoe. Mwaka jana Rainbow Foundation ilipewa Kroner 408.000,- (laki nne na elfu nane) na serikali. Pesa hizo hazijulikani zimeenda wapi. Korir amekuwa akionekana kila siku usiku kwenye sehemu za kunywa.

Rainbow Foundation inachunguzwa na Statens Helsetilsynet (Norwagian Board of Health Supervision) kwa upotevu wa hela hizo.


Chanzo cha habari gazeti la Dagbladet.



4 comments:

Anonymous said...

Wapo wengi tu walio kwenye Police payroll....

Anonymous said...

Korir alikuwa anawadanganya kina dada wa Kiafrika wanaotafuta maisha Norway na kuwashughulikia kiutuuzima ile mbaya na jamaa wengine walikuwa wanaambiwa kuwa watoe cha mbele atawatafutia vibali cha kuishi na kufanyakazi hapa Norway

Egidio Ndabagoye said...

Ebwanaee dah

Anonymous said...

Alikuwa anawalipua watu, Mungu si Athmani, naye wamemlipua!!!!!