Mchakato vazi la
Angela Semaya, Dodoma
Daily News; Tuesday, July 29, 2008 @00:05

Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imesema imekamilisha mchakato kuhusu vazi la Taifa na kwamba itawasilisha rasimu katika baraza la mawaziri kwa ajili ya uamuzi.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Kapteni George Mkuchika alisema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akiwasilisha hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2008/2009.
Alisema rasimu ya waraka wa Baraza la Mawaziri kuhusu vazi la taifa imeshakamilika na kwamba kinachosubiriwa ni kuwasilishwa kwenye baraza la mawaziri kwa ajili ya kufanyia uamuzi.
“Hoja ya kuwapo vazi la taifa letu ni muhimu ndio maana sasa wizara yangu imedhamiria kuufikisha mchakato wa kutafuta vazi la taifa kwenye hitimisho lake,” alisema. Mkuchika alisema mchakato wa kutafuta vazi la taifa ulianza mwaka 2003 kwa kuwashirikisha wabunifu wazalendo na kwamba mwaka 2004 mashindano yalifikia ngazi ya taifa na mavazi 10 bora kwa wanaume na 10 kwa wanawake yalichaguliwa.

No comments:
Post a Comment