Vihiyo si Bongo tu
Jamaa mmoja wa Uingereza kanunua kompyuta kwa Kroner 360,- (Paundi 36,-) kwenye eBay. Jamaa alishikwa na butwaa baada ya kuanza kuitumia hiyo kompyuta. Majina ya wateja, akaunti zao, namba siri za akaunti zao na kiasi cha kila akaunti, namba za Visa na Mastarcard za wateja na saini zao za kawaida na za mtandaoni za wateja wa American Express, NatWest na Royal bank of Scotland. Wateja wengi wa benki hiyo wana mamilioni ya Paundi kwenye akaunti zao.Jamaa angeweza kuzichukua hela zote za hizo akaunti bila ya mtu kujua zimepotelea wapi!!! Jamaa aliyenunua hiyo kompyuta ni bingwa wa TEKNOHAMA, Bw. Andrew Chapman (photo below) wa Uingereza.
Mtaalamu wa TEKNOHAMA, Bw. Adam Laurie ameliambia gazeti la Daily Mail la Uingereza kuwa hiyo ni sawa na kumpa mtu usiyemjua kama ni mwizi au la, funguo na anwani ya nyumbani kwako na kumwambia aende akachukue chochote anachotaka!
Mfanyakazi wa zamani wa kampuni moja ya kuhifadhi data ya Graphic Data aliiuza kompyuta bila ya kufuta data zilizohifadhiwa kwenye hiyo kompyuta.
Serikali ya Uingereza imeanza uchunguzi

2 comments:
Lililomtokea jamaa kuuza hiyo LapTop bila kufuta data ni somo kwetu sote!!!
Wuuuuuuu wiiiiiiiii...kama siri za wateja zinaweza kuvuja kirahisi hivyo, twafa!!!
Post a Comment