Uthibitisho kuwa
mumeo ana kimada
na namna ya
kumkamata.
Uhali gani shosti wangu. Karibu sana katika muendelezo wa makala hii. Leo nakuja na mbinu nyingine ya kupata uthibitisho yakinifu kuwa huenda mumeo akawa na mwanamke mwengine nje zaidi yako, ofkoz na namna ya kumkamata.
4. Pata uhakika kupitia marafiki zake.
Inawezekana kupata ukweli kwa njia hii.
Kwanza ni vyema ukafahamu kuwa kama mumeo ana mwanamke mwingine na wewe hujui basi inawezekana kuwa marafiki zake wanajua. Mwaname atakufichia wewe siri hii ama watu ambao wanaweza kukuletea taarifa lakini hujisikia huru kuwaambia rafiki zake. Na hao marafiki zake, huwa na kasumba ya kuwafichia siri rafiki zao.
Ni kama cheni. Wenyewe wanayaita mambo ya kiume. Na kama hivyo ndivyo basi usitegemee rafiki zake wakwambie kuwa mumeo anakusaliti.
No comments:
Post a Comment