Wednesday, August 20, 2008

Masharti magumu

kuupata uraia

wa Norway

kuanzia 1.9.2008




Unataka kuwa Mnorwejiani?


Kuanzia Septemba Mosi mwaka huu, masharti yameongezwa kwa watakaotaka kuomba ili wawe raia wa Norway. Inalazimu mwombaji ahudhurie kozi ya lugha ya Kinorweji kwa masaa 300. Vinginevyo mwombaji anatakiwa afanye mtihani wa lugha ya Kinorweji na afaulu. Kozi ya lugha ya Kinorweji inagharimu Kroner 15.000,- (kuminatanoelfu) ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania 3,209,660.- (milionitatunalakinimbilinaushee) au Dala za Kimarekani 2,768.- Halafu mwombaji anatakiwa alipe kwanza Kroner 2.500,- (elfumbilinamiatano) kabla ya kupewa uraia.

Sharti lingine kubwa, mwombaji lazima aukane uraia wake wa asili (Norway hairuhusu kuwa na uraia wa nchi mbili).

Sharti lingine: mwombaji awe na rekodi nzuri. Asiwe mefanya kosa lolote la jinai.

Sharti lingine: Mwombaji awe ameishi Norway si chini ya miaka saba.

Sharti la kujua lugha ya Kinorweji, linawahusu wale watakaomba vibali vya kudumu vya kuishina kufanya kazi hapa Norway. Hili linawahusu walioomba vibali vya kuishi baada ya Septemba Mosi 2005.

Chanzo cha habari: Gazeti la jioni la Aftenposten Aften, Jumanne 19.08.2008


No comments: