Saturday, August 09, 2008

Pinda hapingiki





na Mwanne Mashugu

KWA mara nyingine tena, maandamano ya kumpinga Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, yaliyopangwa kufanyika Zanzibar kesho baada ya kupata kibali, yamepigwa marufuku.

Taarifa ya kupigwa marufuku kwa maandamano hayo, ilitangazwa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakar Khatib Shaaban na kuthibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NRA kilichoandaa shughuli hiyo.

Hatua hiyo ya kupigwa marufuku maandamano hayo inakuja wakati watu wasiojulikana wakiwa wametengeneza fulana zenye maneno yasemayo; ‘Zanzibar ni nchi’, ambazo zilitarajiwa kuvaliwa na watu mbalimbali hiyo kesho wakati wa maandamano.

Polisi katika taarifa yake ya jana, ilisema uamuzi wa kuyazuia umetokana na kuwapo kwa taarifa za kubadilika kwa lengo la msingi la maandamano hayo na kuwa kumpinga Waziri Mkuu, Pinda.

Kwa mujibu wa maelezo ya polisi, NRA walipewa maelekezo yaliyowataka kufanya maandamano ya amani, ambayo yasingegusia kabisa hoja inayohusu hadhi ya Zanzibar.


No comments: