Tuesday, August 05, 2008

Shaggy kwenye

Tamasha la

uzinduzi wa Zain

Ijumaa 08.08.08

Dar es Salaam



*Kutoa tiketi 1,000 bure, wakali kibao kumsindikiza

Na Sophia Ashery

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain inatarajia kutoa tiketi za bure 1,000 kwa mashabiki zitakazowawezesha kuhudhuria tamasha la muziki litakalopambwa na mwanamuziki wa hip hop na dance hall kutoka Marekani, Richard Orville 'Shaggy'.

Tamasha hilo linatarajia kufanyika Ijumaa katika viwanja vya Leaders Klabu ikiwa ni tamsha maalumu kwa ajili ya kusherehekea uzinduzi wa kampuni hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Costantine Magavilla alisema tamasha hilo ni moja ya matamasha ambayo kampuni yake imepanga kuyafanya na kuwa Shaggy atatumbuiza moja kwa moja akiwa na bendi yake.

Alisema mwanamuziki huyo ataambatana na wanamuziki 16, ambapo atatumbuiza kwa kupiga nyimbo zake mpya na za zamani ambazo zimempatia umaarufu.

Alisema mbali ya Shaggy wanamuziki wengine watakaopamba tamasha hilo ni pamoja na Rashid Abdalah 'Chid Benz', Hamis Mwinjuma 'Mwana FA', Joseph Haule 'Profesa Jay', Nameless na Wahu kutoka Kenya na kundi la Obsession kutoka Uganda.

Wasanii wengine ni pamoja na pamoja na TMK Wanaume Halisi linaloongozwa na Juma Nature na Wanaume Family linaloongozwa na Amani Temba.


Chanzo: Majira

No comments: