
si nchi, ni ncha
MACHI 17 mwaka 2005, Balozi Ali Abeid Karume (58), ambaye ni mtoto wa hayati Abeid Amani Karume, alipokuwa jijini Mwanza, alisema hivi: “Karume (baba yake) na Nyerere, ndio waasisi wa nchi hii.” Hapa, Balozi Karume, alitaka kuwaambia Watanzania kuwa Bara na Zanzibar ni nchi moja.
Yeye, alifika Mwanza siku hiyo akitokea Musoma mkoani Mara, ili kuomba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamdhamini, apate kuteuliwa kuwa mgombea wakati huo wa Uchaguzi Mkuu.
Ali Karume, wakati huo alikuwa akiwania uteuzi wa mgombea urais wa CCM, uliompa ushindi Rais Jakaya Kikwete, alikuwa Balozi wa Tanzania (si Zanzibar) nchini Ujerumani.
“Mimi ni mtoto wa pili wa hayati Karume,” alisema Balozi Karume, huku akifafanua alivyotembea jumla ya mikoa 18 ya Tanzania (Bara na Visiwani), ili kusaka wadhamini ambao wangemwezesha kupitishwa na chama chake kuwa mgombea.
No comments:
Post a Comment