
Vijana wakidumu hadi
wanadumaa, vijana
chipukizi tutasikilizwa
na nani?
Bongo
Mpenzi Frank,
VIPI harakati zako shujaa wa maisha yangu? Unaukata na harakati zako au zinakatika? Maana vitu vinavyopanda bei sijui mnaishije huko. Juzi nilikwenda kutumia vijisenti vyangu vya kufanya kazi kwa mabosi kumnunulia mama sukari kidogo maana Marieta (si unamkumbuka?
Alitutangulia darasa moja. Kumbe na yeye ni binti wa mabosi nyumba ya nne kutoka kwa bosi wangu). Basi, mama yake Marieta, mgonjwa ndiyo maana anaenda nyumbani. We! Nilidhani nitaweza kumfurahisha mama kidogo, kumbe niliweza kuambulia kilo tatu za sukari na kakhanga kamoja tu. Kumbe kasi mpya maana yake ilikuwa kasi mpya ya bei! Kasi ya kupaa huku sisi tunaning’inia chini tukimwomba Mungu tusije tukadondoka moja kwa moja. Naomba umwelezee mama asije akaona mwanaye anakula starehe kumbe vijisenti havimudu kabisa kasi hizo.
No comments:
Post a Comment