Wednesday, August 27, 2008

Visa kadi zafungwa!



Ujumbe mfupi kutoka Santander Consumer Bank kwa wateja.

Kadi kadhaa za visa zimefungwa kwa muda kwa sababu ya uwezekano kuwa "zimeibiwa kutoka kwenye database" ya Santander Consumer Bank. Ujumbe huo unasomeka (Tafsiri ya Kiswahili)

"Kwa sababu za kiusalama, tumefunga kadi yako ya VISA. Tutakutumia PIN-koda (code) na kadi mpya kwa kipindi cha wiki moja kuanzia sasa. Kama una swali piga namba hii...........Wasalamu wako, Santander Consumer Bank"

Benki imethibitisha kuwa kweli kumwekuwepo na kuibiwa kwa data kwenye "database" yako na benki zingine hapa Norway. Msemaji wa Santander, Bi. Nina Nordby aliliambia gazeti mtandao "Nettavisen" kuwa mpaka sasa hawajui ukubwa wa "wizi" huo, hivyo basi wameamua kufunga kadi za VISA za wateja wao.

Chanzo cha habari: http://www.nettavisen.no



No comments: