Monday, September 29, 2008



Ikiwa leo ni siku ya 68 tangu ‘supastaa’ wa Bongo Flava, Khaleed Salum Mohamed ‘TID’ ahukumiwe kifungo cha mwaka mmoja jela, mwanamuziki huyo amelieleza Ijumaa Wikienda matukio yote ya ukatili anayotendwa ndani ya Gereza la Segerea, Dar es Salaam...



Waandishi wetu walimtembelea TID Jumapili ya Septemba 21, 2008 kwenye Gereza la Segerea anakotumikia hukumu yake ambapo pamoja na mambo mengine, staa huyo aliuita ukatili anaotendewa kuwa ni ufirauni uliokubuhu.

Akitoa ushirikiano wa kutosha kwa mapaparazi wetu, TID alisema kuwa ndani ya gereza wafungwa hawaongozwi na mfumo wa haki na sheria, hivyo wenye ‘mbavu nene’ wanaweza kuwafanya lolote akina hohehahe.

Kufuatia hali hiyo, TID au Top In Dar alisema kwamba katika kipindi chote alichokaa jela, hakuna hata siku moja aliyotabasamu zaidi ya kushinda na mawazo, kulia na kuugulia maumivu yanayotokana na vipigo kutoka kwa wababe wa jela.

“Nilivyoingia humu Segerea wababe wa gereza walinishangilia, wakasema mimi ni mtoto wa mama, usiku walinivamia na kunifanyia mambo yasiyofaa, sasa hivi inanibidi nimtumikie nyapara, nateseka” alisema TID na kuongeza:

"Wababe walinipiga utadhani nina ugomvi nao, walionesha wazi kuwa walikuwa na hasira kali juu yangu. Nikashangaa kwa sababu walinifanyia mpaka vitu vingine ambavyo ni aibu kusimulia.”


3 comments:

Anonymous said...

Halafu waziri wa mambo ya ndani, Masha hivi karibuni alinukuliwa n a vyombo vya habari kuwa "hakuna vitendo vya ufirauni wala vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye jela za Tanzania.....

Zephania Musendo na TID "Top In Dar es Salaam" wanatoa ushahidi ambao watu wote waliofungwa jela za Tanzania wanasimulia!!!!!

Viongozi wa Tanzania wanawafanya Watanzania kama watoto wadogo...

Anonymous said...

NAMWONEA HURUMA TID MBABE MMOJA KESHAMFANYA MKE WAKE....MASKINI WEEEE!!!! POLE...HATA AKITOKA..SIJUI ATAWEZA MAMBO AU NDIO ATAKUWA KESHAHARIBIWA????

Anonymous said...

Huyu jamaa kweli akitoka jela na kurudi uraiani na watu wakimwomba kweli atakuwa na ubavu wa kuwakatalia? Na kila mtu anajua kuwa jamaa ni "mtoto wa mama"

Pole sana TID na yanayokukuta Segerea!!!