Monday, September 01, 2008
ALOZI wa Italia nchini, Fransesco Catania anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo maarufu ndani na nje ya Tanzania, Miriam Julius Odemba, huku ikidaiwa kuwa, wapo katika harakati za kufunga ndoa...
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, balozi huyo amekuwa hajiwezi kwa ‘dada’ yetu huyo kwa mapenzi mazito anayoyapata kiasi cha kumfanya asione soo kwenda naye kwenye ‘kiwanja’ chochote jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ‘matanuz’.
Chanzo chetu cha habari kiliendelea kusema kuwa, uhusiano wa kimapenzi wa wawili hao, umekuwa siyo siri tena kwani wamekuwa wakionekana wakifurahia maisha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na hata ‘mikao’ wanayokaa ni ile inayotambulisha kuwa ni wapenzi.
“Ukweli ni kwamba, yule balozi ‘amedata’ kwa Miriam Odemba, kwani hakohoi wala hafurukuti. Kila sehemu wapo wote wakipeana raha tena hadharani,” kilisema chanzo chetu.
Ili kujua ukweli wa habari hizo, gazeti hili lilifanya jitihada za kuwasaka wawili hao ili waweze kuzungumzia sakata hili, bila mafanikio.
Hata hivyo gazeti hili linaendelea kuwasaka wawili hao, ili waweze kuzungumzia madai hayo
Kutoka GlobalPublishers (Tanzania)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
JAMANI CHA AJABU KITU GANI?
MWACHENI MTOTO WA WATU,YOTE KHERI BORA MAISHA AWE BALOZI,MZUNGU,MWAFRIKA YOTE MAISHA.NA ODEMBA SI MTOTO MDOGO KAKUTANA NA WENGI SI TANZANIA ,ULAYA, AMERIKA NA DUNIA MZIMA, MWACHENI ALE MAISHA YAKE:
Post a Comment