Thursday, September 18, 2008

Nchi ya amani kwa

wanaume tu!


Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Jamani shoga pole,

Nasikitika sana siwezi kupata likizo mara moja na kuja kwako niwe na wewe kwa wakati huo.  Yaani kwa kweli sijui kwa nini wanene wanatung’ang’ania twende tukajifungue katika mavituo yao wakati huduma zenyewe ziko hivyo.  Ina faida gani?  Au ni kwa kuwa wanajua ni njia ya wafanyakazi wao kuongeza mishahara yao wasije wakagoma na kuvuruga mtindo wao wa kujinenepesha?  Pole shoga, pole sana.  Nashukuru tu kwamba wewe ni mzima na ninao uhakika Mungu atakupatia tena ulichonyang’anywa na binadamu na uzembe wao. Tena safari hii utapata na yule unayempenda si yule ibilisi!

Bofya na endelea>>>>>


No comments: