Mzanzibari
aliyekamatwa na
FBI kwa ugaidi
Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwao maeneo ya Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, huku akionekana mchovu, alisema alikamatwa na makachero wa FBI nchini Somali mwaka 2003 akiwa katika shughuli zake za kibiashara na kuingizwa katika gari bila ya kufahamu anapopelekwa.
Akielezea mkasa uliomkuta akiwa eneo la Abusasu, Mjini Mogadishu alisema baada ya kukamatwa na kuingizwa katika gari hilo huku akipata kipigo kutoka kwa maafisa
hao alisafirishwa hadi Nairobi, Kenya na kutakiwa apeleke mtu wa kumdhamani, lakini aliwaambia kuwa yeye ni Mtanzania na kwamba hana ndugu yeyote jijini humo.
No comments:
Post a Comment