
Vihiyo
BOT:
Mambo
baado!
Siku moja tu baada ya kuburuzwa kortini kwa watumishi wanane wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT, kutokana na tuhuma za kughushi vyeti ili waajiriwe na taasisi hiyo, imedaiwa kuwa zoezi hilo litaendelezwa katika taasisi nyingine nyeti ambako inadaiwa watoto na ndugu wa vibosile wameajiriwa kiujanja-ujanja bila kuwa na sifa.
Habari zilizolifikia gazeti hili zinadai kuwa, vigogo kadhaa wako hatarini kuumbuliwa kutokana na ukweli kuwa, katika Benki Kuu peke yake, wako watumishi zaidi ya 12 ambao inadaiwa wamechomekwa kiujanja ujanja.
Imedaiwa kuwa watumishi hao ama ni watoto au jamaa wa vigogo.
No comments:
Post a Comment