Nakaaya Sumari
WANNE WAFUNGUA DIMBA LA KUAGA
Siku chache baada ya kuanza kwa shindano hili, ‘Ijumaa Sexiest Girl’ wasomaji na wapenzi wengi wameonesha kulipokea kwa shangwe, jambo linalowafanya waendelee kutuma meseji za kumwaga, wakiwapigia kura wale ambao wanadhani wanastahili kuendelea kuwepo shindanoni. Kama tulivyowahabarisha wiki iliyopita kuwa, shindano linatakiwa lianze rasmi na warembo 12 kati ya 20 waliyopo pichani, lakini kutokana na wengi kufungana katika kura zao, juzi wanne wametolewa, Nakaaya, Queen David, Violeth na Latoya (waliyowekewa alama ya X) ambao wameambulia kura chache. Bado tunaendelea kuwatafuta 12, unachotakiwa kufanya msomaji ni kuendelea kututumia ujumbe mfupi (SMS) kupitia simu zile zile 0784-275 714, 0787-110 173, utuambie nani anastahili kuingia rasmi katika mpambano huo.
No comments:
Post a Comment