
Bora hata ufuska kuliko ndoa
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
POLE sana mpenzi wangu kwa msiba. Yaani dada yako amefariki dunia! Siamini! Nakumbuka tulivyoishi naye shuleni. Ingawa alikuwa mbele yetu miaka miwili, daima alikuwa mwema kwangu.
Sasa hayupo tena. Ama kweli dunia imegeuka. Itakuwaje kijana kama yeye afariki, tena akiwa na mtoto mdogo? Poleni sana, sana, sana.
Na mtu asiniambie kwamba ni matakwa ya Mwenyezi Mungu. Mungu anataka watu wafe kwa sababu ya uzembe wa sisi binadamu? Mungu anapanga wengine wawe wazembe au walafi ili anayemtaka afe! Sikubali kabisa. Ingekuwa nchi yetu inaendeshwa tofauti dada yako wala asingefariki!
No comments:
Post a Comment