Wednesday, October 22, 2008

Kutoka maoni ya wasomaji

gazeti la Tanzania Daima

la mtandaoni la jana.



Jamani pia angalieni jinsi CCM wanavyofanya uchafu ndani ya TTCL licha ya ule uchafu wa Richard wa Monduli katika Tanesco. Chadema kwa udhaifu huu wa CCM hakika mtashinda. jipeni moyo pia mtafute point kwa wadau

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Salaam,


Mheshimiwa,

Kwa heshima kubwa napenda kukutarifu kuwa hali ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ni mbaya sana baada ya waendeshaji SAKATEL kutoka nchini CANADA waliopewa kuiongoza Kampuni yetu kuamua kwa makusudi kabisa kuihujumu KAMPUNI hii.

Mheshimiwa,

Historia ya kuifisidi TTCL ilianza mwaka 1999 baada ya Serikali ya awamu ya tatu kuanza mchakato wa kuuza 35% ya TTCL kwa wawekezaji wa nje. Katika mchakato huo Serikali iliingizwa mkenge na Watanzania wenzetu walioamua kwa makusudi kujinufaisha kupitia nyadhifa zao. Wahusika wakuu katika mchezo huo walikuwa ni Waziri wa Mipango na Uchumi, Waziri wa Fedha, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi na Mwanasheri Mkuu wa Serikali.


Katika kutimiza azima yao hiyo, Waheshimiwa hao waliingia Mkataba na MSI na DETACON wa kununua 35% share za TTCL. Wawekezaji hao ambao mwanzo ilidaiwa kuwa wanatoka UHOLANZI, kumbe haikuwa kweli bali ni Wajanja wa Tanzania wakishirikiana na Mfanyabiashara mmoja huko SUDAN alikuja kutambulika baadae kuwa MOHAMED SAID IBRAHIM (MSI) ndio waliohusika na mchezo huo mchafu.


Baada ya kukamilisha ujanja huo, wawekezaji DETACON wakaondoka kinyemela na kuiacha TTCL kuongozwa na MSI feki.Muda mfupi baadae HESABU za TTCL zikaanza kuhujumiwa na kutoa taarifa za upotoshaji kwamba KAMPUNI ina hasara na hivyo MSI haiwezi kununua hisa hizo kwa bei waliokubaliana na Seikali ya 120 Million US DOLLARS. Badala yake wakatengengeneza Dili na Mawaziri hao tuliowataja hapo nyuma na wakafanikiwa kuishawishi Serikali ya awamu ya tatu kukubali kuuza 35% kwa bei ya US DOLLARA 60 Million. Baada ya hapo ikapokelewa taarifa kuwa mtoto wa Waziri wa Mawasiliano wakati huo alipelekwa kusoma UINGEREZA na hao MSI feki.

Mheshimiwa Raisi kuanzia hapo TTCL ikawa inaliwa shs 600 Million kila mwezi na jamaa hao wa MSI feki.Piga mahesabu mwenyewe Mheshimiwa Rais, Fedha hizo zimeliwa kwa miaka 4 na hatimae ikaimarishwa CELLTEL.

Baada ya kukamilika CELLTEL, bwana MOHAMED SAID IBRAHIM akauza Kampuni yake kwa mfanyabiashara mwenzie kwa KUWAIT na kupelekea kubadilshwa jina na kuitwa Celtel International na sasa ZAIN.Hapo serikali machale yakawacheza na kuamua kuzitenganisha Kampuni hizo mbili CELLTEL na TTCL.

Mheshimiwa Raisi, ulipoingia madarakani, Serikali yako ikatafuta mwendeshaji mwingione wa kuongoza TTCL kutokana na makubaliano yenu na CELTEL INTERNATIONAL.Katika mchakato huo ikapatikana SASKATEL kutoka CANADA.

Serikali yako iilifikiri imetatua tatizo la TTCL kumbe hao mawaziri waliotajwa hapo juu ndio walioshiriki tena katika mchezo mchafu na kupatikana SASKATEL feki kama ilivyokuwa MSI fake.

Mheshimiwa Raisi, wanachokifanya SAKATEL hivi sasa ni kuihujumu TTCL kwa lengo la kuijenga Kampuni mpya ya HITS mabayo wenyewe ni hao mawaziri waliohusika kuiteketeza TTCL hulo nyuma.

Hujuma za moja kwa moja zinazofanywa na SASKATEL kwa maelekezo ya Mawaziri hao ni kuhakikisha TTCL haiendi mbele kwa kufanya yafuatayo:

1.Wamesimamisha Matangazo yote ya Biashara ya TTCL.

2.Wamesimamisha Miradi yote ya TTCL.

3.Wamesimamisha kutafuta Wateja wapya (Marketing) kwa TTCL

4.Wamesimamisha ununuzi wa spare za mitambo ya TTCL

5.Wameamua kubana matumizi kwa asilimia 30 ya mapato ya TTCL.

6.Business Plan ya TTCL iliyotengenezwa na Wazalendo imepelekwa kampuni ya HITS.

7.Wametengeneza Salary Structure ya kuwa-frustrate Mafundi wa simu TTCL ili waache kazi au wagome.

Katika Structure hiyo, Wafanyakazi wa Idara ya Biashara wenye Elimu ya Darasa la saba na kumi nambili wanalipwa mshahara wa shs 1,100, 000.

Wafanyakazi Mafundi wenye Elimu ya Form VI, FTC na Diploma wanalipwa shs 600,000.

8.Chief wa Mauzo na Masoko Mama Lorein, anaendesha mkakati wa kuwarubuni Wataalamu wote wazuri wa TTCL waende Kampuni ya HITS.

9.Huu mwezi wa pili hawajapeleka michango ya Wafanyakazi katika mifuko ya Hifadhi ya jamii NSSF na PPF

10.Huu mwezi wa pili hawajapeleka fedha za michango ya SACOS za Wafanyakazi wa TTCL katika chama chao cha Kuweka na Kukopa


Mheshimiwa Raisi, jamaa hawa mpaka sasa wameendesha mradi wa kudai madeni ya TTCL yanayofikia shs 65 Billion.Wameshakusanya 15 BILLION LAKINI HAZIONEKANI NDANI YA ACCOUNT ZA TTCL.

Katika kubana matumizi wameserve 3 Billion kila mwezi kuanzia October 2007 hadi sasa lakini nazo hazimo kwenye account za TTCL.

Wameleta wataalamu ambao wanalipwa 800 kila mwezi kwa kazi ambazo zinazweza kufanywa na Wazalendo.

MHESHIMWA RAISI TUNALETA KWAKO UTUSAIDFIE TWAFA.
Wako,

Mbwana Muungwana.

Kwa niaba ya Wafanyakazi TTCL


No comments: