Mwisho wa Ramadhan
usiwe mwanzo
wa maovu
Mhariri
Daily News; Wednesday,October 01, 2008 @11:47

KIPINDI cha mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhan ndiyo kimemalizika kwa Waislamu kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri ambapo huwa ni siku ya furaha na kujumuika na familia.
Katika kipindi cha mfungo huo wa Ramadhan, tulishuhudia watu wakifuata maamrisho ya dini ya Kiislamu, walikuwa watulivu na kufanya ibada ipasavyo, hali tunayoiona ni nzuri si kwa dini tu ya Kiislamu bali hata kwa hali ya ubinadamu.
Tukiangalia uzoefu wa miaka iliyopita, baada ya kumalizika mwezi huu mtukufu tu watu waliokuwa wasafi na wenye maadili mema ya dini, huwa wanarejea katika maovu ikiwamo ujambazi, wizi na kutoa lugha chafu za matusi.
Kwa upande wetu, tunawasihi wote waliokuwa katika mfungo na kufuata maadili mema waendelee nayo na wasirejee katika maovu tena kama dini ya Kiislamu inavyoamrisha lakini pia kwa ajili ya amani ya nchi yetu na kwa kuzingatia ubinadamu.
Iwapo watu hawatakubali kuendeleza yale mazuri waliyokuwa wakiyafanya wakati wa Ramadhan ni wazi siku hii ya Idd tutashuhudia vitendo vingi vinavyotokana na maovu kama ajali, ujambazi na hata kusababisha watu wengine kupoteza maisha.
Mfano kwa mujibu wa dini ya Kiislamu hairuhusiwi mtu aliyefunga kunywa pombe siku ya Idd ya kwanza na iwapo atakunywa maana yake funga yake yote imepotea hivyo mtu asipofuata hilo na kunywa pombe nyingi si anapoteza maana ya funga yake bali pia anaweza kuleta maafa kwa wengine.
Kuna usemi usio rasmi kuwa baada ya Ramadhan tu, kumbi za starehe kama disko zinajaa, gesti nazo zinafurika, kwenye baa nafasi za kugombania, majambazi wanaibuka tena. Kauli hii inaonyesha kuwa maovu yanaibuka tena, tunawaomba wale walioweza kujizuia na haya basi waendelee na si kurejea tena.
Amani, maadili mema ikiwamo wanawake kujisitiri mitaani, uhalifu kuwa wa kiwango cha chini na kuwarahisishia kazi polisi wetu wanaolinda amani ni miongoni mwa mambo yaliyotawala wakati wa Mfungo wa Ramadhan, tunaomba hali hii iendelee.

No comments:
Post a Comment