Monday, November 24, 2008

Anna Kilango:

aitaka serikali

kuwakamata na

kuwafikisha mahakamani

wamiliki wa kampuni

ya Kagoda Agriculture Ltd



Mheshimiwa Mbunge Anna Kilango Malecela


Na Simon Mhina

Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, ameitaka serikali kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wamiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd pamoja na makampuni mengine yaliyoshiriki kuchota fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hata kama wamezirudisha. 

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kilango alisema wakati anaipongeza serikali kwa kupiga hatua moja ya kuwafikisha mahakamani baadhi ya watuhumiwa, lakini inapaswa kupiga hatua nyingine ya pili ya kuwaburuza mahakamani wahusika wote. 

Mbunge huyo alisema uamuzi wowote wa kutowafikisha mbele ya mahakama watuhumiwa wote bila kujali wamerudisha fedha hizo, ni kinyume cha sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katiba ya Jamhuri ya Muungano..

..bofya na endelea>>>>>

No comments: