Dk. Hoseah:
Mafisadi wananitishia
maisha
Na Exuper Kachenje MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea ameeleza kuwa amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa watu mbalimbali wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi. Hoseah amekuwa akitoa kauli za kijasiri katika siku za karibuni, ikiwemo kauli yake ya mapema wiki iliyopita kuwa iwapo serikali itawakamata kwa wakati mmoja watuhumiwa wote wa kashfa ya EPA, nchi inaweza kuyumba na juzi alitamka bayana kuwa wale wanaodhani vigogo hawapandishwi kizimbani kwa tuhuma za rushwa, wasubiri mwezi ujao. Katika mahojiano na Mwananchi baada ya kufunga Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Mapambano Dhidi ya Rusgwa kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dk Hoseah alisema kuwa katika siku za karibuni amekuwa akipokea simu za vitisho na matusi kutoka kwa mafisadi, ingawa hakutaja ni kundi gani la mafisadi wanaofanya vitendo hivyo. Hoseah alisema kuwa vitisho hivyo vimekuwa vikitolewa kwa nyakati tofauti na watuhumiwa hao ambao hutumia njia ya simu na ujumbe mfupi wa maandishi wa simu (sms)....bofya na endelea>>>>> |
1 comment:
Mhhh aya bwana yetu macho tu wabongo.
Post a Comment