Warioba aonya amani
Tanzania inayoyoma
Asema viongozi wanakumbatia matajiri, nchi inahitaji maadili mapya ya viongozi
Na Ramadhan Semtawa
WAZIRI MKUU mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameonya kuwa iwapo hali ilivyo sasa nchini ikiachiwa iendelee kama ilivyo, amani, umoja na utulivu vitatoweka.
Kauli ya Jaji Warioba ambaye anaheshimika kutokana na maono yake ya mara kwa mara kuhusu mwelekeo wa nchi, imekuja wakati nchi inakabiliwa na tatizo la ufisadi na migomo kutoka kwa makundi mbalimbali ya jamii.
Huku akichambua nchi ilikotoka, ilipo na inakoelekea, Jaji Warioba alionya jijini Dar es Salaam jana kwamba, hakuna tena sera ya kujitegemea bali msingi wa maendeleo ni fedha, huku utu ukitoweka kwa kasi kubwa na kwamba, hali hiyo imeibuka zaidi baada ya kuvunjwa Azimio la Arusha visiwani Zanzibar mwaka 1990....bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment