Saturday, December 13, 2008


Badala ya kupaza sauti kwa

kuimba ‘UHURU’ kila mmoja

amwulize mwenzie ‘u huru?’



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,


MAMBO leo mpenzi?  U huru leo?  Wajionaje uliyezaliwa ndani ya nchi huru huku nchi huru inasherehekea? 

Mimi ni mzima wa afya lakini kama kawaida nina wazimu wa akili pia maana mambo ninayoyaona hapa yanatosheleza kumpa mtu wazimu moja kwa moja.  Kweli mpenzi. 

Waweza kufikiria kweli kwamba wanene wa nchi hii wanalalamika eti hawako huru.  Kwanza, niliposikia hivyo, nilimkumbuka mwalimu wetu wa historia.  Si yule mwenye ndevu aliyejidai kwamba ni mwanamapinduzi hadi wakaja watu kutoka wapi sijui na kumwambia kwamba akiendelea kudai hivyo watamponda hadi ashindwe kujipinda.  

Eti hakuna haja ya mapinduzi wakati chama chenyewe kimemaliza mambo yote ya mapinduzi tayari.  Mapinduzi mengine ni uhaini tu. ..bofya na endelea>>>>>


No comments: