Matokeo ya urafiki
wa Marekani na
jamaa wa FFU ameshika
bunduki ya Kimarekani
Askari wa kikosi Maalum cha kutuliza ghasia (FFU) akiwa kamili kabisa kuhakikisha hali ya
Usalama katika moja ya mitaa jijini Dar es Salaam kufwatia sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, ulinzi umezidi kuimarishwa karibu kila kona ya jiji huku askari wakiwa wamesheheni silaha mbalimbali na nzito kukabiliana na hali yoyote..
Huyu askari wa FFU ameshika bunduki rasharasha ya Kimarekani ya aina ya M-16.
Anaonekana kama jamaa wa US Marines au jamaa wa US Navy SEAL jinsi alivyovaa. Hata ushikaji wa bunduki si kama ule wa zamani. Ushikaji huu wa bunduki ni wa majeshi ya Kimarekani! Haya ni matokeo ya urafiki kati ya Marekani na Tanzania.
Chanzo kutoka kwa mdau Hakingowi
No comments:
Post a Comment