Membe:
CCM inajimaliza
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinajimaliza chenyewe kutokana na kuendekeza makundi ndani yake.
Alisema uzoefu alionao, unaonyesha kuwa vyama tawala haviondolewi madarakani na vyama vya upinzani, bali hujiondoa vyenyewe kwa kutokuwa makini na kuendekeza makundi, chuki, fitina, majungu na migogoro isiyo na tija.
Alisema kwa sasa CCM inatafunwa na makundi na kusababisha mgawanyiko miongoni mwa wanachama, jambo ambalo likiachwa liendelee, linaweza kukimaliza chama hicho tawala.
Membe alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, uliofanyika jana katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
Katika uchaguzi huo uliotawaliwa na vituko vya kila aina, mtoto wa Mbunge wa Viti Maalumu, Tatu Ntimizi, Said Ntimizi, aliibuka mshindi na kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, hivyo kupata nafasi ya kuingia katika Baraza Kuu la UVCCM.
Alisema ndani ya CCM kuna makundi yanayokua kila kukicha, hususan ndani ya jumuiya za chama na kushusha heshima ya chama hicho....bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment