Thursday, December 18, 2008


Tunachezeshwa uchi

Uarabuni!!!!




Mariam Mndeme na Amina Salim

Mmoja wa wanenguaji maarufu nchini aliyewahi kufanya kazi na bendi mbalimbali ambaye ni miongoni mwa wasichana waliowahi kwenda Uarabuni kwa kazi ya unenguaji ametoboa siri ya kwamba, baadhi ya wanaokwenda huko huchezeshwa uchi kwenye makasino.


Akiongea na Amani kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini mnenguaji huyo alisema kuwa, wengi wanaokwenda huko kwa kazi hiyo ya kukata mauno ni kweli wanapata mikataba ya muda mfupi ya kufanya kazi hiyo na bendi za huko lakini akafichua kuwa, baada ya shoo kuna wanaochukuliwa na kwenda kuchezeshwa kwenye majumba ya starehe na kupewa ‘mshiko’.

Aidha, mtoa habari huyo alifafanua kuwa si wote wanaokwenda huko wanafanya hivyo bali wenye tamaa ya fedha ndio hufurahia tenda hizo za udhalilishwaji
“Ukweli ni kwamba, tunapokwenda Uarabuni tunaitwa kwenda kufanya kazi, lakini baada ya shoo kuna ambao wanachukuliwa na kwenda kuchezeshwa uchi kwenye makasino kwa ujira mnono,” alisema mnenguaji huyo. 

Baada ya kupata nyepesi hizo, Amani lilifanya mahojiano na baadhi ya wanenguaji wengine waliowahi kwenda kunengua katika falme za kiarabu ambao walikanusha shutuma hizo huku wakidai kuwa zina lengo la kuwachafua.

Mmoja wa wanenguaji hao ni Aisha Mbegu ‘Madinda’ ambaye kwa upande wake alikiri kuwa amekuwa akienda Dubai kwa kazi hiyo ya unenguaji lakini akaeleza kuwa yeye si miongoni mwa waliowahi kufanyiwa vitendo hivyo vichafu.

“Habari hizo kasema nani? Ni kweli huwa tunakwenda huko kunengua kwasabau waarabu wanapenda sana show za Wanenguaji wa Bongo lakini sio katika Makasino,”alisema Aisha.

Naye mnenguaji maarufu na wa siku nyingi ambaye hivi karibuni aliwahi kwenda Uarabuni kwa kazi hiyo Queen Suzy alipoulizwa juu ya shutuma hizo alieleza kwamba, wanaodai kwamba wanaokwenda Uarabuni wanakwenda kuchezeshwa uchi ni wale wenye chuki binafsi wanaotaka kuwaharibia wenzao.


Chanzo: Global Publishers (TZ)

No comments: