BAKWATA yataka
Mapumziko ya mwaka mpya
wa Kiislam!!!!
BARAZA Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) limepeleka maombi serikalini kutaka siku ya mwaka mpya wa Kiislaam iwe sikukuu ya kitaifa.
Sambamba na hilo Bakwata imeomba siku hiyo iwekwe katika kalenda ya serikali na iwe ya mapumziko na kufahamika katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Suleiman Gorogosi alisema maombi hayo walishayapeleka serikalini tangu mwaka jana.
"Maombi yetu tumeshayapeleka kwa serikali tangu mwaka jana kupitia kwa waziri mkuu aliyepita Edward Lowassa ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mwaka jana, tunachotaka ni kupata kibali cha kupata mapumziko ya sikukuu hiyo ili iwe kama sikukuu nyingine na kufahamika katika jamii,"alisema Sheikh Gorogosi.
Gorogosi alisema kuwa mwaka 1429 ambao (leo) jana ni tarehe 28/12 Hijjiria (sawa na Desemba 27 mwaka huu, hivyo wanatarajia kuingia mwaka mpya wa Kiislam 1430 ambayo Jumatatu Desemba 29, 2008...bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment