Thursday, December 25, 2008



Western Union

yazindua promosheni




na Chalila Kibuda

KAMPUNI ya huduma ya kutuma fedha ya Western Union, imezindua promosheni ya mwisho wa mwaka inayojulikana ‘Go East African, itakayowanufaisha watumiaji wa huduma hiyo.

Akizungumza na waandishi jana, Mwakilishi wa Benki ya Posta, Kolimba Tawa, alisema promosheni hiyo itaendelea mpaka Febrauri 28 mwakani.

Alsema Western Union kwa kushirikiana na mawakala wake hapa nchini, wamebuni promosheni hiyo ambayo washindi watajishindia zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 35. Mawakala wa Western Union ni Benki ya Posta, Diamond Trust Bank, KCB na BOA 
“Hii ni aina ya kwanza ya promosheni kama sehemu ya kuwapatia hamasa watumiaji wa huduma kuendelea kutumia Western Union katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuweza kupata zawadi kwa kile wanachokitumia,” alisema Tawa.

Alisema katika droo ndogo washindi 15 kila mmoja atapata fedha taslimu sh milioni moja wakati katika droo kubwa washindi watano watapata fedha taslimu sh milioni nne kila mmoja.

Alisema mbali na zawadi ya fedha, washindi 30 katika droo ndogo watapata zawadi za simu za mkononi na wakati katika droo kubwa washindi 40 watajishindia simu hizo kila mmoja.

Kutoka Tanzania Daima


No comments: