Monday, January 19, 2009

Chuo Kikuu D´Salaam

Balaa tupu!


Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo asubuhi wamekamatwa na polisi baada ya kukutwa na mabango yenye maneno ya uchochezi wakati wa usaili wa wanafunzi waliotakiwa kudahiliwa chuoni hapo. Waliokamatwa ni Bahati Alone, Issah Paul, Titus Ndulah na Sabinian Prins Pius.

LEO UTATUELEZA
CHUO KIKUU LEO NOMA TUPU
Mmoja wa wanafunzi akipelekeshwa msobemsobe na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), mara baada ya kukamatwa.

LEO HAKUNA UTANI
CHUO KIKUU LEO NOMA TUPU
Huyu naye naye akipelekwa kwenye ‘difenda’ kwa ajili ya kupelekwa lupango.

TANGANYIKA JEKI ILIPOFANYA KAZI
CHUO KIKUU LEO NOMA TUPU
Msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, akipigwa ‘Tanganyika Jeki’ mara baada ya kukamatwa.

RAHA YA DIFENDA UINGIE MWENYEWE
CHUO KIKUU LEO NOMA TUPU
Mwanafunzi huyu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akipanda Difenda tayari kupelekewa mahabusu.

MOJA YA MABANGO YALIYOKAMATWA
CHUO KIKUU LEO NOMA TUPU
Hili ni moja kati ya mabango waliyokamatwa nayo wanafunzi hao.

BANGO JINGINE LILILOKAMATWA 
CHUO KIKUU LEO NOMA TUPU 
Bango hili nalo lilikamatwa

HAPA HACHOMOKI MTU
CHUO KIKUU LEO NOMA TUPU

CHUO KIKUU LEO NOMA TUPU
Wanafunzi waliokamatwa wakiwa chini ya ulinzi mkali ndani ya Difenda ya FFU.
PICHA RICHARD BUKOS /GPL.

Picha na habari kwa hisani ya Global Publishers Tanzania


No comments: