Na Mwandishi Wetu
Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mwanaidi Mbaraka (20) yuko chini ya ulinzi mkali wa polisi baada ya kukinyonga kichanga chake alichojifungua katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na baadaye kukidumbukiza kwenye ndoo iliyojaa maji ya kutawazia.
Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na Mwandishi wetu, lilitokea Desemba 31, mwaka jana, ambapo binti huyo ambaye ni mfanyakazi wa ndani aliamua kukikamata kichanga chake na kwenda msalani kabla ya kukinyonga na kukidumbukiza kwenye ndoo hiyo ya maji.
Awali yaya (mfanyakazi wa ndani) huyo alifikishwa hospitalini hapo Desemba 30 na Baba mwenye nyumba (Jina tunalo) baada ya kupata uchungu wa kujifungua.
Imeelezwa kwamba baada ya kufikishwa wodi ya wazazi siku iliyofuata Desemba 31, majira ya saa 6 mchana, msichana huyo alifanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume, ambaye alionekana mwenye afya njema.
Habari zaidi zilizidi kueleza kwamba ilipofika majira ya saa 4, usiku wa Desemba 31, aliupokea mwaka 2009 kwa kufanya ukatili wa kumuua mwanaye huyo mchanga.
Imedaiwa kwamba siku ya tukio msichana huyo aliwachenga wakunga na kufanikiwa kuingia chooni na kichanga chake ambapo alipofika chooni alijaza maji ndoo kisha akakitumbukiza kichanga hicho kwenye ndoo hiyo.
Baada ya kufanya unyama huo msichana huyo alirudi kitandani akaendelea kuuguza maumivu, kabla ya muda mfupi baadaye wauguzi kushtuka baada ya kumuona akiwa hana mtoto.
Wakunga hao walipofanya uchunguzi walikikuta kichanga hicho kikiwa kinaelea kwenye ndoo ya maji kikiwa kimeshafariki tayari.
Watu waliohojiwa na mwandishi wetu wamelaani vikali kitendo hicho na kukiita cha kinyama.
“Huyu mama kafanya unyama mkubwa kwa kichanga hiki katika Mwaka huu wa 2009,” alisema mama mmoja ambaye naye alifanikiwa.
No comments:
Post a Comment