Si mafisadi wamo ndani ya
kundi la Wabunge. Kwa hiyo,
kwa mantiki ya uganga,
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
ASANTE sana kwa barua yako tamu kama ahadi za wanasiasa mpenzi! Nafurahi sana kuona kwamba umeshinda mdudu wivu na kuelewa kwamba mimi ni wako, wako, wako. Maana mpenzi huwezi kujua jinsi nilivyosononeka wiki jana. Mpaka mama bosi akatishia kunifukuza kazi.
‘We Hidaya, una maana gani kununanuna namna hii? Kama hutaki kazi si useme tu. Hii ni mara ya tatu kwa wiki moja umeacha maziwa yaungue huku huna habari kabisa.’
Nilijaribu kumpooza lakini sikutaka kumwambia sababu ndiyo maana akazidi kunitishia. Sasa baada ya kupata barua yako, kidogo nirukeruke kama ndama na ninao uhakika MB alishangaa. Atajiju.
Lakini mambo zaidi mpenzi? Pole sana ya kuumwa tumbo na sasa tutaumwa kichwa, tumbo na kila kitu baada ya kimbilio letu kupigwa marufuku....bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment