Friday, January 30, 2009




Mfuko wa pensheni wa Taifa

waondoa hisa zake

Barrick Gold ya Canada,

inayomiliki migodi ya

Bulyanhulu




Mfuko wa pensheni wa taifa wa Norway "The Government Pension Fund/Statens pensjonsfond", umeondoa hisa zake zote toka kwenye kampuni kubwa ya migodi duniani, Barrick Gold baada ya kashfa kadhaa zinazozihusu Barrick Gold na kampuni moja ya Kimarekani, the American Company Textron Inc. Moja ya kashfa kubwa ya Barrick Gold ni ya mauaji ya wakazi kadhaa wa Bulyanhulu yaliyafanyika miaka kadhaa iliyopita na serikali ya Tanzania kukataa kufanya uchunguzi wa mauaji hayo, pamoja na mauaji hayo kumekuwa na migogoro kadhaa baina ya wakazi wa maeneo ya karibu na migodi hiyo na wamiliki wa migodi hiyo. Barrick Gold inamiliki migodi.

Sababu nyingine ya kujitoa mfuko wa pensheni ni uchafuzi wa mazingira kwenye makampuni ya migodi inayomilikiwa na Barrick Gold, nchini Papua New Guinea.

Kujitoa kwa mfuko wa pensheni wa taifa wa Norway toka Barrick Gold ni pigo kwa kampuni hiyo na wachunguzi wa mambo wanahisi mfano wa Norway unaweza kuigwa na nchi zingine, hususani za Skandinavia.

Chanzo cha habari: Norwegian TV 2

http://vcr.csrwire.com/node/12629


http://www.africafiles.org/article.asp?ID=19871


http://www.radiomundoreal.fm/rmr/?q=en/node/26891


http://gregornot.wordpress.com/2009/01/06/uprising-against-barrick-gold-in-tanzania/


http://www.corpwatch.org/article.php?id=15263



http://www.minesandcommunities.org/article.php?a=8263

No comments: