Sakata la hijabu Norway.
Waziri wa sheria atoa
uamuzi wa mwisho..
hakuna kuvaa
hijabu wala ushungi!!!
Kofia ya jeshi la polisi la Norway.
Waziri wa sheria wa Norway, Bw. Knut Storberget ameamua kutupilia mbali pendekezo lililotolewa na Inspekta Jenerali mkuu wa polisi, Bi. Ingelin Christine Killengreen la kuruhusu wanawake watakaopenda kuvaa hijabu au ushungi kwenye jeshi la polisi. Bw. Storberget amefikia uamuzi huo, baada ya kujulikana kuwa, mshauri wake wa kisiasa, Bi. Hadia Tajik na katibu mkuu wa wizara ya sheria, Bi. Astri Aas-Hansen waliamua kukubali mapendekezo ya Bi. Killengreen na kutangaza uamuzi huo kwenye tovuti ya wizara, bila ya kumwarifu. Storberget imebidi asitize likizo yake ya majira ya theluji na kurudi kutetea unga wake.
Wanasiasa wa vyama vya upinzani wanamtaka Bw. Storberget ajiuzulu kwa kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo. Storberget amekataa kujiuzulu...
No comments:
Post a Comment