Saturday, February 21, 2009



Uthibithisho yakinifu kuwa

mumeo ana mwanamke

nje na jinsi ya kumkamata




Mambo vipi shost wangu. Leo spendi kupoteza muda kuamkia hapa kwani niliyonayo ni mengi moyoni nataka niyatue hapa. Kama umfuatiliaji najua, unajua kuwa wiki iliyopita nilikuahidi kukuletea muendelezo wa makala hii.

Unakumbuka nilitaja dalili ambazo zinaweza kukuhakikishia kuwa mumeo ana mwanamke nje...! Nikakuasa usijiaminishe kwani kwa mwanamme lolote laweza kutokea. Nikajaribu kukupa dalili 12 ambazo zitakuwezesha kujua kuwa mumeo ameanza huo mchezo ama laa.

Tayari ulikuwa na wasiwasi, na kuna vitu vilikwambia akilini kuwa hii sio kawaida yake lazima kuna mtu anayejaribu kuingia baina yenu.

Inawezekana ulihisi hivyo kutokana na mabadiliko uliyoyaona siku za hivi karibuni, au labda inaweza ikawa ni kutokana na kauli zake, ama umehisi mabadiliko katika mwenendo wake wa maisha siku za hivi karibuni.

Nikasema inawezekana kwa asilimia kubwa kuwa ukawa uko sawa kabisa...

Kwa sababu hisia za namna hii mara nyingi ni za kweli. Uliziangalia hizo dalili ukawa na uhakika wa asilimia mia moja kuwa anakutenda.

Lakini bado nikakwambia kuwa muda wa kumwambia kuwa unajua kila kitu haujafika. Nikakutaka usubiri. Bila shaka siku saba ulizosubiri zilikuwa nyingi na ndo maana leo hapa staki kupoteza muda.

Shoga Wanaumme ni wagumu kukubali unapojaribu kuwakabili katika hili suala tena bila vithibitisho vya uhakika. Tena ataruka asilimia mia moja na kukufanya ujione mjinga kwa uongo atakao utumia kuprove kuwa hajakutenda ill'hali unajua moyoni kuwa amekutenda.

Leo nakupa mbinu 10 za kupata uthibithisho yakinifu kuwa mumeo ana mwanamke nje na jinsi ya kumkamata... ukifanikiwa shosti hachomoi, niamini.

1. Chunga simu yake...

Anapopokea simu ukiwa naye angalia jinsi anavyoongea na hiyo simu, je anaonekana hajiaminiamini hivi? anaongea kama mwenye haraka ya kutka kukata? Anoongea kwa uchache sana kisha anakata! au utaskia mmmh, eeeh, sawa. ok kisha anakata. Hee! huyo si mwingine bali ni mwizi wa penzi lako.

Chakufanya...

Usimkurupukie hapo hapo na wala usimuulize.... Subiri mpaka ajisahau, chukua simu yake wakati yeye hajui, nenda kwenye incomming calls, utainasa hiyo namba.

Nenda kwenye miss calls angalia kama ipo tena. angalia receiced calls. Nenda kwenye msg. angalia msg zenye namba hiyo. Angalia msj yoyote ambayo huielewi chukua namba. Endelea kuchunguza msj zake kwa kipindi fulani.

Unaweza ukutane na namba ambayo ameisevu kwa jina la kiume, lakini ukawa na wasi wasi nayo, tafuta simu nyingine weka private namba kisha piga, sikiliza sauti inayopokea... ni sauti ya kike, walaaaaaaa! umemnasa, usiongee chochote katika simu hiyo, endelea kuifuatilia namba hiyo. Chunguza saa na muda wa maongezi anaoutumia kuzungumza na namba uliyonawasiwasi nayo. Weka kumbukumbu.

Anaweza akawa mjanja, (Mwizi smart) anaweza akawa anafuta namba zote zilizoingia na kutoka kabla ya kuingia kulala. Tik!. hiyo niishara kuwa kuna namba anazificha. Anaweza pia akawa ameitia loki simu yake, jaribu kumuuliza kwanini na angalia jinsi anavyojieleza. Mpaka hapa utakuwa umemnasa. Namna ya kumkabili...! Bado! subiri kwanza.

Hicho ni kithibitisho kimoja tu. itaendelea wiki ijayo. Usikose

Kutoka gazeti la Mwananchi


No comments: