Monday, March 09, 2009


Athari za utandawazi





Maskini Tanzania! Sifa mbaya ya wawekezaji wa Kichina nchini, imeendelea kuchukua nafasi pana, baada ya hivi karibuni Ijumaa Wikienda kubaini biashara ya ngono, inayoendeshwa kama duka ndani ya hoteli ya kifahari jijini...

Duka hilo la ngono lipo ndani ya hoteli inayoitwa Chinese Massage & Hotel, iliyopo Mtaa wa Ndovu, Mikocheni, Dar es Salaam ambapo watoa huduma ni warembo wa Kichina.

Biashara hiyo, inafanyika bila kificho na bei imepangwa maalum kwa wanaohitaji huduma ya penzi la Kichina ambayo ni Dola za Marekani 100 au shilingi 135,000 kwa mtu anayelipa kwa noti za nyumbani.

Huduma nyingine ambayo hutolewa kwenye hoteli hiyo ni ya kuchua (massage) ambayo gharama yake ni shilingi 40,000.
Wiki iliyopita, gazeti hili lilitonywa na chanzo chake kuhusu kuwepo kwa uwekezaji huo wa ngono ndani ya hoteli hiyo na kulitaka kufika kujionea ili liweze kuwaokoa Watanzania na ‘msiba’ huo.

“Fikeni mkajionee wenyewe, mimi nimekwenda pale na nimeona hali halisi. Ukifika tu, unaulizwa waziwazi unataka huduma ipi kati ya ngono au massage, yaani hakuna kificho kabisa,” alisema mnyetishaji wetu.

Baada ya kupata ‘data’ hizo, Jumatano iliyopita Ijumaa Wikienda lilituma mpelelezi wake ambaye kama ilivyoelezwa awali, alipofika Mapokezi aliulizwa huduma anayohitaji kati ya ‘masaji’ na ngono.

Mpelelezi wetu, alimjibu mrembo wa Kichina ambaye alimkuta Mapokezi kuwa anahitaji huduma ya ngono na kutajiwa bei yake kuwa ni dola 100, kisha akaomba kuwaona watoa huduma hiyo ili kujiridhisha kama wanafaa au la!

Kama ilivyo kwa msemo wa ‘Mteja ni Mfalme’, dada wa Mapokezi aliwakusanya warembo wanne wa Kichina ‘fasta fasta’ na kumuonesha mpelelezi wetu ambaye alidai ameridhika nao, hivyo kuahidi kurejea majira ya alasiri siku hiyo.
Wakati wa kuondoka, mpelelezi wetu aliomba kadi ya biashara (Business Card) yenye namba zao za simu ili iwe rahisi kuwapata pindi atakapohitaji.

Bila hiyana wala hofu yoyote, dada yule wa mapokezi alimpatia business card ambayo ina anuani ya mahali hoteli hiyo ipo na namba za simu za mkononi, ambazo ni 0797 168 997 na 0763 585 196.

Kwa kutumia namba ya simu, 0763 585 196, Ijumaa Wikienda lilianzisha mawasiliano ya ujumbe mfupi wa maneno (sms) na watu wa hoteli hiyo, likiulizia kama kuna warembo wapya wameingia, ili liweze kufika na kujitwalia mmoja wa Kichina wa kufanya nao ngono.

Baada ya kuulizia hilo, zilipita kama dakika 10, ndipo upande wa pili ukajibu pia kwa njia ya sms kuwa yupo mmoja.Gazeti hili baada ya kujibiwa hivyo, liliuliza tena kiasi cha fedha ambapo safari hiyo jibu halikuchukua muda mrefu kuwa ni dola 100.

Mazungumzo hayo kwa njia ya sms, yalikuwa kama ifuatavyo;
Ijumaa Wikienda: Hi, have you news girls in your shop? I need one for sex today. (Habari, kuna warembo wapya? Nahitaji mmoja wa kufanya naye mapenzi leo)

0763 585 196: Yes have new girl, welcome (ndiyo, yupo mpya mmoja karibu)
Ijumaa Wikienda: How much to pay for that new girl? (Nitampata huyo msichana mpya kwa bei gani?) 

0763 585 196: 100 dollars (Dola 100)
Ijumaa Wikienda: Can’t I use Tanzania Shillings to pay? (Siwezi kutumia fedha za Kitanzania?)
0763 585 196: I’m sorry, 135,000 Tshs. (Samahani, Shilingi za Kitanzania 135,000)

Ijumaa Wikienda: I’ve only 120,000 and I’m may way there. (Nina 120,000 tu, na nipo njiani nakuja)
0763 585 196: 120,000 Tshs is ok. (120,000 sawa)

Gazeti hili, baada ya kufanya uchunguzi huo, lilikwenda moja kwa moja kwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Mark Kalunguyeye na kumpa ‘data’ kamili ambapo aliahidi kulisambaratisha duka hilo la ngono kwa kutumia rungu la dola.

Ijumaa Wikienda bado lipo bega kwa bega na RPC Kalunguyeye katika kuhakikisha Wachina hao wanakomeshwa. Soma Gazeti la Ijumaa, litakalotoka Ijumaa ya wiki hii ili kujua matokeo zaidi.
 

1 comment:

Anonymous said...

Mko dunia gani?Kipi cha ajabu?