
Hivi ni mfadhili, fedhuli
au mfanyadili?
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
Ewe mwenye imani ndogo jamani. Kwa kuwa sikuwepo ulipopiga simu juzi tayari unafikiri mimi fisadi wa mapenzi? Ni haki hiyo kweli. Mama Bosi kanituma supasoko wakati huohuo nasubiri simu yako, sasa nimkatae? Vibaya hivyo mpenzi. Wajua nakupenda kwa moyo wote lakini wivu wa ‘fimbo ya mbali’ achana nao. Mi wako Bwana nikuambie mara ngapi!!
Tena nilikuwazia kwelikweli juzi maana hawa wanaojiita wafadhili wakajileta kwa bosi jioni. Kumbe kwao wao, hakuna mheshimiwa wala mwishiwa, labda tu kiwango cha pesa kitachoongelewa. Nakumbuka wewe na kikundi chako mlivyoandika proposa kwa mafadhili kumbe mafedhuli wanaojidai kuunga mkono ujasiriamali wa vijana. Proposa ilikuwa nzuri sana hadi mafedhuli wote walikuwa tayari kutoa pesa. Yaani mpenzi, kila nikikumbuka nataka kulia. Mwandike nyinyi, mfanye kazi nyinyi mwingine afaidi kwa kuwa tu yeye ni mtoaji
No comments:
Post a Comment