Thursday, March 05, 2009


Kwani bastola ni dhambi

au kuua ndiyo dhambi?




Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.



Mpenzi  wa enzi
Japo huna Benzi,
Natamani kukuenzi,
Kwa bonge la tenzi
Ila mama bosi mshenzi
Atanitia kwenzi.



Na hapo ndipo ushairi wangu unakwisha.  Nashangaa.  Nilivyokuwa malkia wa ngonjera huko shuleni, siku hizi yamenikimbia kama mtu mwenye kipindupindu.  Vipaji vinapotea hivihivi.  Lakini wakati wote naendelea na urais wangu wa fagio, nakuimbia nyimbo lukuki kichwani mwangu.  Laiti ungesikia mpenzi nadhani hata wewe ungefurahi.  Hujambo lakini?  U mzima au umegeuka wazimu kutokana na ahadi rahisi na hali ngumu?

Mimi sijambo kama kawaida yangu.  Angalau siwezi kupata magonjwa ya ajabuajabu kutokana na mazoezi makali ya ufagio kila siku.  Wiki jana nilishindwa kumaliza barua kwa sababu niliitwa ghafla maana wageni walikuwa wamekuja bila kutarajiwa. 

Unajua mpenzi, maisha ya mnene aliyechaguliwa,  hata wakija watu saa ngapi lazima awahudumie kwa kuogopa kukosa uhondo wa kuweka sponji zako kwenye sponji za Dodoma.  Lakini wageni wakiondoka, si malalamiko hayo! bofya na endelea>>>>>


No comments: