Liverpool yaivuruga
Man. United
Liverpool 4
Manchester United 1
Liverpool imerudisha matumaini upya ya kuwa mabingwa wa England, baada yakuwanyuka wapinzani wao wa jadi, Manchester United kwa magoli 4 – 1 kwenye uwanja wa Old Trafford (Uwanja wa ManU.)
Manchester walipata goli kwenye dakika ya 23 lililofungwa na Christiano Ronaldo. Dakika ya 28, Torres alitumia mwanya wa kosa la mlinzi wa ManU, Vidic na kusawazisha goli. Kuanzia hapo Liverpool wakicheza kwa uhakika zaidi, walianza kutawala uwanja!
Dakika ya 44, Gerrard alifunga goli la pili la Liverpool.
Dakika ya 77, Aurelio, Mbrazili wa Liverpool alipiga ”frikiki” kutoka umbali kama wa mira 20 hivi na Van der Sar, golikipa wa ManU, aliuangalia mpira ukitinga nyavuni!!!
Dakika ya 90, Dossena, alifunga goli la 4 la Liverpool.
Manchester United:
Edwin van der Sar, John O`Shea, Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Patrice Evra, Cristiano Ronaldo, Michael Carrick, Anderson, Ji Sung Park, Wayne Rooney, Carlos Tevez.
Marizevu:
Ben Foster, Dimitar Berbatov, Ryan Giggs, Nani, Paul Scholes, Jonny Evans, Darren Fletcher.
Liverpool:
Pepe Reina, Sami Hyypia, Jamie Carragher, Martin Skrtel, Fabio Aurelio, Javier Mascherano, Lucas Leiva, Dirk Kuyt, Steven Gerrard, Albert Riera, Fernando Torres.
Marizevu:
Diego Cavalieri, Alvaro Arbeloa, Andrea Dossena, Ryan Babel, Emiliano Insua, David Ngog, Nabil El Zhar.
Refarii: Alan Wiley
Imetumwa na mpenzi wa Liverpool, Mtambalike wa Oslo.
No comments:
Post a Comment