Tuesday, March 24, 2009


Mambo 25

yanayokufanya

uwe Mswahili... !!!!




na Alex Mukurasi,
University of Dar es Salaam
Computing Centre
Source: Tanzanet Mailing List
list@tanzanet.org


1.Unamwita mtu usiyemjua(wala kuonana nae kabla) Anti au Anko au Sista ama
Braza.

2.Asilimia 90 ya CD pamoja na kanda za cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki au ni za kuazima.

3.Chumba chako kimejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k.

4.Una machupa ya maji matupu ya shampoo na perfume pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu wala huna shughuli navyo.

5.Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali, chidi,mamu, dida, Ngunyi, Songoroo n.k.

6.Hakuna mtu katika Familia yako anayetoa taarifa kwako anapokuja kukutembelea mfano kaka,shangazi n.k..

7.Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.kulivyochukua sehemu kama vile mgahawani.

8.Mama yako ana migogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa miezi 10 au zaidi.

9.Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano usiku sana)na mara nyingi huwa una beep tu. Na uki-beep unaangalia salio..

10.Ulipokuwa mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi.

11.Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa.

12.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi asingekuwa vile yule..

13.Unapenda kuhudhuria / kushiriki hafla na sherehe mbalimbali kama vile harusi, maulidi, Ubarikio n.k ambazo hujaalikwa na wala huhusiki.

14.Unapenda kuomba kununuliwa dola (credit), pombe, soda, sigara n.k

15.Unapoingia katika chombo cha usafiri unapenda kupigania/kukimbilia na hata kuingilia dirishani..

16.Unapohudhuria hafla au sherehe fulani unapenda kubeba bia, maji, soda na chakula kupeleka nyumbani wakati unarudi.

17.Unapenda kutembelea watu ovyo ovyo hata kama hujaitwa au huna jambo la msingi linalokufanya la kukupeleka kwao.

18.Unapenda kuongea saana kuhusu mambo ya watu wengine (Umbea), mara sijui fualni kafanya hivi, mara fulani hana lolote...

19.Unapenda sana kuongea unapokuwa na watu lakini maongezi yenyewe hayana msingi wowote, ili mradi tu uonakane nawe umo.

20.Unapenda sana kusoma magazeti ya udaku, kama vile Kiu, Ijumaa n.k. na pia habari zisizokuwa na elimu ndani yake. Kama vile Baba Ubaya, Toto tundu, Babu suni n.k.

21.Unakuwa mbishi sana kutoa michango ya harusi, ila kwenye mnuso wewe ndio wa kwanza kufika na wa mwisho kuondoka tena ukiwa ndiiiiiii....

22.Unaiga kila kitu toka kwa jirani yako badala ya kubuni mambo yako. Mfano akifungua grocery we nawe unafungua yako ubavuni, akifuga kuku, we nawe umo....

23.Unakuwa huendi out na mkeo na kama mkienda shughulini yeye hutangulia mbele kabisa na wewe unafuata nyuma kwa mbali kama watu baki, na huko mkifika hakuna kujuana. Ukionekana out na mtu basi ni nyumba ndogo

24.Unakuwa kila jambo la kila mtu kazini kwako unalijua, lakini la kwako hakuna anayelijua. ukiulizwa unakuwa mkali kama mbogo

25.Una tabia ya kuandaa pilau na kuku wakati wa sikukuu tu. Halafu mayai, matunda na maziwa unakula ama unaandaliwa ukiwa umelazwa hospitali

NOTE:- Wapelekee na wengine ili wajue ni kitu gani kinawafanya kuitwa Waswahili... ......kama Mimi na Wewe.


No comments: