Gazeti hili la Uwazi ambalo lilikuwa la kwanza kuripoti habari za mtoto huyu lilimfuatilia mtoto huyu hadi shule anayosoma ili kujua maendeleo yake kitaaluma na mahusiano yake na wanafunzi wenzake.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita Christina Emmanuel ambaye ni mwalimu wa darasa analosoma Baraka alisema kwamba mtoto huyo amekuwa akifanya vizuri sana darasani katika masomo yake hivyo kuwa tishio kwa wanafunzi wenzake.
Mwalimu Christina aliendelea kusema kwamba, Baraka amekuwa na uwezo wa juu katika masomo ya Hisabati, Sayansi, Kiingereza na Kiswahili na ni mmoja kati ya wanafunzi wanaofanya vizuri darasani.
Aidha mwalimu huyo alisema kwamba, licha ya kufanya vizuri katika masomo, pia anaonekana ni mwenye kipaji cha uongozi kutokana na kuwa akiwatuliza wanafunzi wenzake darasani ili wasipige kelele jambo ambalo amekuwa akilifanikisha kwani amekuwa akisikilizwa, hivyo muda wote kumekuwa na utulivu.
“Tangu ameletwa hapa shuleni alionekana mwenye kipaji hali iliyotufanya tumrushe darasa ambapo anasoma la pili hivyo la kwanza hakupitia lakini amekuwa akifanya vizuri sana tofauti na jinsi wengi walivyokuwa wanafikilia kuwa hawezi kwa kuwa ameishi porini na wanyama kwa kipidi kirefu” alisema mwalimu Christina.
Kuhusu tabia yake Darasani, Mwalimu Christina amesema kuwa, huwa mara nyingi anakuwa ni mwenye furaha na hupenda sana kushirikiana na wananfunzi wenzake na amekuwa akiomba msaada wa mwalimu bila kuona aibu.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi Selesia Mgendela, alisema kwamba mtoto Baraka ana tabia ya kupitia ofisini kila anapofika na kuondoka shuleni kwa lengo la kumuamkia.
“Nawashukuru sana wananchi ambao wamekuwa wakimsaidia kwa misaada mbalimbali jambo linalomfanya Baraka ajisikie vizuri.”alisema mwalimu mkuu huyo
Aliendelea kusema kwamba ni vigumu kuamini kuwa mtoto ambaye aliishi Porini na Wanyama kwa kipindi kirefu kufanya vizuri kimasomo darasani.
Mtoto Baraka aliokotwa porini akiwa na Nyani aliyekuwa akimlea sambamba na watoto wake wengine baada ya kutupwa na mama yake mzazi akiwa angali mchanga.
Hata hivyo aliachana na maisha ya porini baada ya maafisa wa wanyamapori kumpiga risasi hadi kufa Nyani huyo mlezi hali iliyompelekea mtoto Baraka naye kujeruhiwa kwa risasi mguuni.
Baraka hadi leo amekuwa akihuzunishwa sana na kuuwawa kwa Nyani huyo aliyempenda kama mzazi wake kwani mpaka sasa hawajui wazazi wake.
Baada ya kuuwawa kwa Nyani huyo maafisa wa wanyamapori walimchukua mtoto Baraka hadi kijijini ampapo inasemekana kwa siku za mwanzo alikuwa hawezi hata kuongea kama binadamu wa kawaida, na alikuwa akitembea kwa miguu na mikono kama wafanyavyo Nyani.
Mtoto Baraka alichukuliwa na mfanyabiashara mmoja, Rose Mbwambo kwa lengo la kumsaidia na kuja kuishi naye jijini Dar es Salaam ambapo hadi sasa anaishi maeneo ya Tabata Kimanga.
Tuesday, March 03, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment