Wednesday, March 25, 2009


Utendaji wa kazi

wa polisi Tanzania



Hivi ni kweli polisi wanahitaji mpaka Waziri Mkuu awaambie kuwa vibaka wanavuta bangi pembezoni mwa ukuta wa Ikulu ndo wakurupuke na kuanza kamatakamata?
 
Je huo ukamishina wanaupataje, kwa nguvu za giza au kwa kusimama Salenda ili wakubwa wakipita wawaone au kwa kuzuia daladala zisiwagonge wakubwa wanapopita na misafara yao mirefu?
 
Hivi kweli ni sawa Wachina waanze kuandamana kwa kuwa nchi hii kwa sasa sio salama tena kwa
wawekezaji? Je ile nishani aliyopewa mkuu wa Idara ya operesheni maalumu katika jeshi la Polisi alipewa kwa kazi ya kukamata wapika gongo, kazi ambayo hata mgambo wa kijiji anaweza kufanya au alipewa kwa kuwapiga mabomu Chadema kule Tarime?
 
Je Polisi ni wataalamu wa kupambana na watu wasio na madhara tu kama wanafunzi wa Chuo? Je Polisi wameridhika na kazi ya kuwa maripota wa matukio ya Ujambazi na wanaoua Albino badala ya kuwakamata?
 
Je
  Inawezezekana baada ya miaka yote hii Wizara ya Mambo ya Ndani haijaweza kupata mtendaji mzuri kama Mzee Lyatonga?
 

Inasikitisha, Inasononesha, Inakatisha Tamaa na Inatia hasira.


Tuesday, 24 March, 2009 9:21 PM

From: James MmM jamesfrequent@gmail.com

To: list@tanzanet.org

Subject: [tanzanet] FWD: Utendaji wa Polisi


1 comment:

Anonymous said...

Mwandishi kafanya kazi nzuri lakini kasahau ya Abdala Zombe na yale mauaji ya likatili yaliyofanywa na polosi Arusha. Kuna Polisi ambo sasa wamekua tishio kwa raia wema. Waziri ajiuzulu mara moja kwani naye anashutumiwa kwa ufisadi. JK apangue jeshi la polosi