Sunday, March 08, 2009



Waziri wa JK afumwa

akifanya ngono garini




Waziri kijana wa serikali ya awamu ya nne, inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, katika Wizara nyeti, hivi karibuni amefanya kinyaa baada ya kufumwa akifanya ngono na mke wa rafiki yake ndani ya gari...


Chanzo cha habari kilisema kuwa, tukio hilo la aibu kwa Waziri huyo, mwenye mke na watoto wawili, lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye maegesho ya Hoteli ya Sea Cliff, Masaki jijini Dar es Salaam, jirani na nyumbani kwake, ambapo mheshimiwa alibambwa ‘laivu’.

Awali ilidaiwa kuwa, Waziri huyo bonge, mwenye nywele ndefu, amekuwa akiwalipa walinzi wa ‘pakingi’ hiyo kiasi cha shilingi elfu tano kila anapotia timu mahali hapo kwa lengo la ‘kugandamiza malavidavi’.

Kilisema miongoni mwa askari hao kulikuwa na mjeshi mgeni ambaye alikuwa hajui ‘gemu’ hilo la mheshimiwa hivyo kulibumburua kirahisi kufuatia kutojua juu ya mshiko unaotolewa na kigogo huyo kwa walinzi wenzake.

Chanzo hicho kilidai kwamba, Waziri huyo mzoefu wa migogoro ndani ya chama chake, alifika katika eneo hilo la tukio kwa kutumia gari ndogo aina ya RAV 4 yenye vioo vyeusi, ambapo iliegeshwa kwa muda mrefu, jambo lililosababisha askari huyo aliyekuwa hajui ‘dili’ kwenda kuangalia kulikoni!

Ilidaiwa kuwa, baada ya mlinzi huyo kumkurupusha mheshimiwa huyo katika maraha na mke wa mshkaji wake, aliondoa gari hilo kwa kasi, na kuondoka katika eneo hilo baada ya kugundua watu wameshtukiwa kamchezo kake kachafu.

Gazeti hili lilikwenda eneo la tukio kwa lengo la kupata ‘a-z’ ya ‘ishu’ hiyo, ambapo kwa mujibu wa mmoja wa walinzi hao, ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alikiri kuisikia skandali hiyo kwa maafande wenzake, huku akionesha kuwa na woga mkubwa katika kuizungumzia.

“Nimesikia kwa jamaa zangu hapa lakini huyo Waziri nasikia ni mtu mkatili sana, kwa hiyo hata mimi namuogopa,” alisema mlinzi huyo huku akimtaka Mwandishi kuondoka eneo hilo.

Aidha, alipotwangwa swali juu ya ukweli kuwa mheshimiwa huyo siku ya tukio alikuwa na mke wa rafiki yake, afande alisema: “Ni kweli mwanamke huyo ni mke wa mshkaji wa kigogo huyo na mara kwa mara hutinga naye hapa hotelini”.

Gazeti la Risasi - Jumamosi 07.03.2009


3 comments:

Anonymous said...

Ajali kazini!!!!

Wengi tu wanazini. Si wanaume si wanawake....

Anonymous said...

Wee unayejiita Dia Gnosis (hiyo so Kigiriki?)


Unaonyesha unapenda sanaa ngono!!!!

Anonymous said...

Huyo waziri ni pashkuna tu...hakuna lolote zaidi ya hapo!