Tuesday, April 14, 2009

Akamatwa na Polisi

Akiendesha Gari Huku

Akifanya Mapenzi



Mwanaume mmoja wa Norway anasubiria faini kubwa na kunyang'anywa leseni yake ya udereva baada ya kukamatwa na polisi akiendesha gari huku akifanya mapenzi na mpenzi wake tena akiwa katika mwendo mkali wa kilomita 133 kwa saa.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye polisi wa Norway waliweka jina lake kapuni alikamatwa akiwa kwenye tendo lenyewe na polisi kwenye barabara kubwa ya E18 kilomita 40 toka Oslo.

Maafisa wa polisi walilinasa gari la jamaa huyo na mpenzi wake Mazda 323 likiwa katika mwendo mkali wa kilomita 133 kwa saa na kabla ya baada ya muda mfupi kugundua kwamba jamaa huyo alikuwa havunji sheria ya speed limit pekee bali pia alikuwa katika shughuli nyingine. 

"Gari yao ilikuwa ikiyumba toka upande mmoja hadi mwingine kutokana na mwanaume huyo kushindwa kuona vizuri mbele kwakuwa walikuwa wakifanya mapenzi mwanaume huyo akiwa amempakata mpenzi wake kwenye mapaja yake wakati huo huo akiendelea kushikilia usukani" alisema afisa mmoja wa polisi.

"Hakuweza kuona mbele kwakuwa mgongo wa mpenzi wake ulikuwa ukimziba kuona mbele, kwanini waliamua kufanya mambo hayo barabarani kwenye hatari kubwa , hatujui"

Baada ya kuwafuatilia kwa umbali wa takribani kilomita moja, mapolisi waliwasimamisha na kuwakamata.

"Tumechukua leseni yake ya udereva kutokana na hatari aliyokuwa akiisababisha" alisema afisa huyo wa polisi.

Adhabu ya dereva huyo itaamuliwa wiki ijayo baada ya waendesha mashtaka kuipitia video ya ushahidi iliyochukuliwa na polisi wakati wa tukio hilo.

Afisa huyo wa polisi alisema kwamba wanategemea dereva huyo atapigwa faini ya maelfu ya Krone za Norway na adhabu ya muda mrefu ya kupigwa marufuku kuendesha gari.


No comments: