Monday, April 27, 2009



Waendesha mtandao

Ze Utamu wasakwa,

Ni baada ya kuwadhalilisha

viongozi



Na Said Mwishehe

JESHI la Polisi nchini limesema linafanya uchunguzi wa kina zaidi ili kubaini wanaojihusisha na mtandao wa kompyuta unajulikana kama  Ze utamu ambao unatumika kudhalilisha watu wakiwemo viongozi wa ngazi za juu.

Hatua hiyo ya Jeshi la Polisi imetokana na kukithiri kwa picha mbalimbali  za kudhalilisha kupitia mtandao huo.

Siku za hivi karibuni mtandao huo umekuwa ukitumia nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari , kudhalilisha viongozi jambo ambalo ni kinyume cha ustaarabu na maadili ya jamii.

Akizungumza na Majira jana kwa njia ya simu mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa  Jeshi la Polisi(jina tunalo) alisema kuwa mtandao huo umefikia mahali ambapo hautavumiliki tena na kazi inayoendelea sasa ni kuwasaka wahusika wake.

"Tumeona jinsi mtandao huo unavyodhalilisha viongozi wetu, sisi kama Jeshi la Polisi hatutavumulia, uchunguzi wa kina umeanza na muda sio mrefu mtasikia nini tumekifanya kwa watu hao,"alisema ofisa huyo.

Mbali ya kuchunguza wahusika Jeshi hilo pia  linafuatilia kwa undani kupata wamiliki wa mtandao huo ambapo kutokana na vitendo vyake hautavumiliwa tena.

Tume ya Mawasiliano Tanzania  ( TCRA), imekiri kuwepo vitendo mbalimbali vya udhalilishaji kupitia mtandao huo na kuahidi kulishughulikia suala  hilo haraka iwezekanavyo.

" Tumeona hili, tunachokifanya sasa (jana mchana) tunakutana  kikao cha dharura kujadili suala hilo kwa undani," alisema mmoja wa maofisa wa Tume hiyo aliyeomba kutoandikwa jina gazetini ambaye pia  hakutaka kufafanua hatua watakazochukua kudhibiti tatizo hilo. 

Wakizungumza na gazeti hili, wananchi mbalimbali walilaani vikali kitendo kilichofanywa na mtandao huo na kutaka upigwe marufuku sambamba na  wahusika wake  kukamatwa mara moja popote walipo na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

"Sisi kama Watanzania, hatubali vitendo hivi vya kipuuzi na fedheha kupitia mtandao huo viendelee vyombo vya dola vichukue hatua za haraka kuwakamata wote wanaojihusisha  na mtandao huo ," alisema  mama aliyejitambulisha kwa jina la Bi. Hawa Majaliwa .

Mwananchi mwingine aliyeomba kutoandikwa jina mkazi wa Upanga jijini Dar es Salaam, alisema hatua iliyofikia na  mtandao huo haivumiliki na itashangaza kama vyombo vya dola vitashindwa kuwanasa wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Iliandikwa kwenye Majira 23.04.2009


4 comments:

Engima said...

Hey. Am sorry for what they said for ourbeloved president but i could help you guys with one thing? i have the acces to the satellite so in a week i can get Mr.Ze Utamu by using the Satellite forum. thats the only thing you can get the person appart from intterogating and negotiating with him.
Regards to my beloved president. Jakaya Kikwete Sorry for what happended

Anonymous said...

engima wala usiombe ruhusa ,we saidia tu huyo jamaa apatikane.Kwa kweli ni aibu kweli.Watanzania tumejivua nguo ,tusilalamike majirani zetu wakitudharau zaidi na zaidi.Aibu am ashamed guys.

Anonymous said...

Mtandao huu wa ze utamu umkuwepo kwa muda mrefu sana na watu wengi wasio na hatia (raia wa kawaida) wamedhalilishwa sana kupita mtandao huo kwa picha zao kuwekwa bila ridhaa yao. nyingi ya hizo picha ni za utupu na hata zile ambazo siyo za utupu ziliwekwa bila ridhaa ya wahusika. hivi kuwekwa picha ya rais Kikwete ndo kila chombo kinachojifanya cha usala kinakurupuka kuwasaka wenye mtandao? kumbe vyombo hivyo vya usalama na udhibiti ambavyo vinaendeshwa kwa gharama kubwa kwa kodi za wananchi walipa kodi vipo kwa ajili ya usalama na maslahi ya viongozi tu. unafiki mkubwa na ufisadi aina nyingine huu. kudhalilishwa ni kudhalilishwa, ama iwe ni raia tu, kiongozi wa kawaida na hata rais.

na sisi tunaoandika maoni yetu kulaani ze utamu sasa, siku zote tuliona sawa tu watu wa kawaida kudhalilishwa katika mtandao huu wa kibazazi, leo kawekwa Kikwete ndiyo mnajitutumua, eti wamevuka mipaka. mipaka hiyo ni ipi na iliwekwa na nani, na nani alitoa maagizo kuwa isivukwe? Unafiki mtupu! siupendi hata kidogo.

Genc said...

engima wala usiombe ruhusa ,we saidia tu huyo jamaa apatikane.Kwa kweli ni aibu kweli.Watanzania tumejivua nguo ,tusilalamike majirani zetu