Thursday, May 28, 2009


Kwa hali hii, bora tuanzishe

Bongo Siasa Search



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.

Waendeleaje na hali? Unajua nakuwazia kila siku ninayoangalia Bongo Star Search. Nakumbuka ulivyotaka kuingia na jinsi tulivyokuhimiza maana tunajua uwezo unao. Lakini kila nikiangalia sasa namshukuru Mungu kwamba ulighairi maana jinsi watu wanavyodhalilishwa humu ... lo mpenzi, nadhani ningevunja luninga wangekusema vile na viburi vyao vya kaburi, na kujidaidai kwao utadhani Miungu wanaojua kila kitu.

Mimi sikatai mpenzi, wako wengine ambao kweli hawajui kuimba, na wako wengine ni wazi hawajajiandaa hivyo wanajikanyaga vibayavibaya. Lakini hiyo inawapa fursa mahakimu wahasimu wale kutukana na kukejeli na kukebehi wapendavyo? Najua wale si wa kwanza kutukana na hata katika mashindano mengine ya vipaji angalau yuko jaji mmoja mchungu lakini safari hii wote ni wachungu kuliko sumu….bofya na endelea>>>>>


No comments: