Wednesday, May 27, 2009


Mtandao wa kuwanasa

walarushwa wazinduliwa



Na Kulthum Maabad 

TAASISI ya Agenda Participation 2000 ikishirikiana na ubalozi wa Finland pamoja na Shirika la Maendeleo la Uswizi imezindua mtandao rasmi wa kukamata watumiaji rushwa. 

Uzinduzi wa mtandao huo unaotambulika kwa jina la Tanzania Corruption Tracker System umefanyika jana katika jijini Dar es Salaam. 

 

http://www.corruptiontracker.or.tz/


Akiendesha mkutano huo ulioudhuliwa na wadau mbalimbali wa vita vya rushwa, Mwenyekiti wa Agenda Participation 2000 Prof Max Mmuya alisema taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2000 kwa lengo la kusaidia kuelimisha watu juu ya upigaji kura na uchaguzi wa haki. 

“Rushwa kama kiumbe hai chenye kukua na kupumua na chenye akili za kutosha hivyo lazima kama Watanzania ambao tunataka maendeleo tukasaidiana kwa kupeana taarifa na kufanya utafiti wa kina kutokomeza kiumbe hicho. 

Balozi wa Finland nchini Tanzania ambae pia alikuwa mgeni rasmi alitaja jududi zaidi za kupiga vita rushwa ili kuhakikisha kwamba misaada inayotolewana nchi wafadhili inatumika ilivyokusudiwa. 

“Bila kutokomeza rushwa tutakuwa tunafanya kazi bure, misaada yeyote inayoletwa nchini kwa ajili ya Watanzania lazima iwafikie walengwa hao,” alisema. 

Naye Balozi wa Uswizi Tanzania, Adrian Schalaepfer akiwa miongoni mwa wageni rasmi siku hiyo aliipongeza Tanzania kwa kujitahidi kutetea haki za watu wake dhidi ya rushwa. 


No comments: