Tuesday, May 12, 2009


Nini nimejifunza kutoka

Zeutamu na ufisadi

  

Zeutamu


1. Wengi walilalamika kuwa zeutamu inawadhalilisha na wakataka ifungwe - hakuna aliyerespond.

2. Wengi walilalamika kuwa zeutamu imevunja ndoa zao na mahusiano na wapenzi wao na wakataka ifungwe - hakuna aliyesikiliza

3. Baadhi wakaandika kuwa kuna watu wamejiua kwa ajili ya zeutamu na wengine wajijidhuru na hata kuathirika kisaikolojia hakuna aliyesikiliza . . . .

4. Na hatimaye Mkuu Wakaya akadhalilishwa . . . . Usalama wa taifa hakuna aliyekuwa na amani, vijana wote wakaingia kazini, Police Force wakaingia kazini, Intelpol wakaingia kazini na hatimaye zeutamu haipo tena. Yote hayo yalifanyika katika muda mfupi sana . . . . . . .


Ufisadi


1. Wananchi wameumia sana miaka mingi kwa ajili ya ufisadi . . . hakuna aliyewasikiliza

2. Wananchi wamekufa sana kwa ajili ya umasikini ambao wakati mwingine umesababishwa na ufisadi hakuna aliyeshtuka

3. Hatimaye orodha ya mafisadi ikatajwa . . . . Matokeo yakaanza kuonekana

4. Hatimaye Mafisadi wakubwa wakaanza kutajwa . . . na sasa mengi yafichuka na yataendelea kufichuka na najua kutakuwa na matokeo.

Just wondering . . . Nchi hii mambo hayafanyiki hadi wakubwa na mafisadi waguswe.

Nimejifunza kuwa ili nchi hii mambo yaende sasa ni lazima kuwagusa wakubwa na mafisadi?

Kama si hivyo . . . hakuna linalofanyika au kutendeka!!!

Imetumwa na Jamaldeen. T. Bin Mazar E. Shariff Ibn Zenjibari

No comments: