Waziri wa utalii Zanzibar
ziarani Oslo kukuza
sekta ya utalii.
Waziri wa utalii, biashara na uwekezaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Bi. Samia Suluhu Hassan, yuko ziarani Norway katika jitihada za kujaribu kutangaza na kukuza sekta ya utalii visiwani. Kwenye ziara ya Bi. Samia inazijumuisha Qatar, Sweden, Norway, Denmark na Urusi. Sambamba na ziara ya waziri wa utalii wa SMZ, pia waziri wa utalii na mali asili wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Shamsa S. Mwangunga, naye yuko ziarani kwenye nchi za Afrika kwa ziara ya kutangaza na kukuza sekta ya utalii ya Jamhuri ya Muungano.
Bi. Samia amezungumza na makampuni ya utalii, makampuni yanayosafiria watalii kwa mkupuo, taasisi na vitengo vinavyohusika na sekta ya utalii na amezungumza pia amezungumza na shirika la ndege la SAS (Scandinavia Airline System) kuona kama pana uwezekano wa SAS kuanzisha usafiri wa ndege kwa watalii (charter flight) kwenda visiwani.
Waziri Samia amepewa changamoto kubwa ya jinsi ya kuboresha sekta ya utalii, kabla ya Waskandinavia hawajaanza kusafiri kwa wingi kwenda Zanzibar na Tanzania bara kama wanavyofanya kwenye jinsi ya jirani Kenya. Mengi ya waliyomwambia, tayari SMZ inayafanyia kazi. Changamoto moja waliyompa na kurekebisha miundombinu ya sekta ya utalii na nchi kijumla.
Akiwa Oslo, amepata bahati ya kukutana na baadhi ya Watanzania waishio Oslo, na viongozi wa kamati ya utendaji wa Chama Cha Watanzania Oslo, kwenye hoteli ya Rica Travels. Kwenye makutano hayo, Watanzania walimwuliza waziri maswali kadhaa ya muhimu yanayoikabili nchi kwa sasa na waziri Samia alionyesha upeo mkubwa wa ufahamu wa mambo kwa kuyajibu maswali ya Watanzania kwa umahiri wa hali ya juu.
3 comments:
hivi mbona wote walioongozana na muheshimiwa ni magabachori hapan ufisadi hapa ?
Hivi rangi ndiyo inayoamua nani Mtanzania halisi? Je, kuwa na rangi hiyo ni alama ya kuwa fisadi? Fisadi ni fisadi tu, haitegemei rangi, kabila, dini wala madhehebu...
ZNZ Road Show Delegation,
You're looking alive and kicking, hopefully you've managed to puul a lot of business for ZNZ...
I would have loved to be in Oslo with you guysw...I'm looking forward to rejoin you all in Moscow on Wednesday...
Take care...
Max SereneT
Post a Comment