Monday, June 08, 2009

Alhaj Omar Bongo,

Rais wa Gabon afariki



Alhaj Omar Bongo.


Habari toka  Agence France Presse na  gazeti la Le Point la Ufaransa, yakikariri habari toka ndani ya serikali ya Ufaransa kuwa kiongozi aliyetawala muda mrefu Afrika, Alhaj Omar Bongo (73) wa Gabon amefariki dunia kutokana na saratani (kansa) mjini Barcelona. Hakuna habari zozote rasmi za kufariki kwa Omar Bongo. Waziri Mkuu wa Gabon, Bw. Jean Eyeghe Ndong, alisema kwenye luninga za Gabon kuwa ameshtushwa na habari hizo na kuwa hana taarifa za kufariki kwa kiongozi wake.

Omar Bongo alikuwa makamu wa Rais mwaka 1967, na kuwa Rais mwaka 1968, baada ya Rais wa kwanza, Leon Mba kufariki dunia. Bongo na mmoja wa marais wa Afrika wanaochunguzwa na serikali ya Ufaransa kwa ufisadi. Wengine ni Dennis Sassaou-Nguesso wa Kongo Brazaville na Teodoro Obiang Nguema wa Guinea ya Ikweta.

Alhaj Omar Bongo alizaliwa Albert Bernard Bongo, lakini mwaka 1973 alisilimu na kuwa Mwislamu. Mkewe, Edith Lucie Bongo (mtoto wa Dennis Sassaou - Nguesso Rais wa Kongo) alifariki mwezi Machi mwaka huu.

Wachunguzi wa mambo ya siasa wanadai kuwa, Ali Ben Bongo (mtoto wake) anatayarishwa kuchukua nafasi ya baba yake. 


No comments: