Monday, June 22, 2009

The boys from Brazil

with a licence to thrill..

Brazil yaibamiza Italia

3 - 0




Mabingwa wa dunia Italia walishindwa kuwika mbele ya Brazili katika mechi ya mwisho ya kundi B la kombe la mabara na kujikuta ikiadhiriwa kwa kucharangwa mabao 3-0.

Magoli yote matatu ya Brazili yalifungwa ndani ya dakika nane za mwisho wa kipindi cha kwanza.

Baada ya kosakosa nyingi langoni mwa Italia, Luis Fabiano aliifungia Brazili goli la kuongoza katika dakika ya 37 baada ya kuachia shuti kali lililojaa nyavu ndogo za kulia mwa golikipa wa Italia Gianluigi Buffon.

Fabiano aliwanyanyua tena washabiki wa Brazili dakika sita baadae kabla ya Dossena kujifunga mwenyewe wakati akiokoa krosi ya Robinho kwenye dakika ya 45.

Kwa ushindi huo Brazili imejikusanyia pointi tisa kwa kushinda mechi zake zote tatu za kundi B.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo mabingwa wa Afrika timu ya taifa ya Misri baada ya kuwafunga mabingwa wa dunia Italia siku ya alhamisi kwa bao 1-0 ilishindwa kuonyesha kiwango ilichokionyesha siku hiyo kwa kukubali kubamizwa 3-0 na Marekani.

Marekani ilikuwa imepoteza mechi zake zote mbili za mwanzo dhidi ya Italia na Brazili.

Magoli ya Marekani yalifungwa na Davies dakika ya 22, Bradley dakika ya 63 na kwenye dakika ya 71 Dempsey alifunga daftari la magoli la Marekani.

Kwa matokeo hayo Misri imetupwa nje ya mashindano hayo baada ya kushika mkia kwenye kundi B.

Italia nayo imeyaaga mashindano hayo baada ya kuzidiwa kwa tofauti ya magoli na Marekani.

Marekani sasa itakiputa na Hispania kwenye mechi ya nusu fainali wakati Brazili itakabana koo na wenyeji Afrika Kusini.

No comments: